Mtunzi: W. Kiwango
> Mfahamu Zaidi W. Kiwango
> Tazama Nyimbo nyingine za W. Kiwango
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Willy Kiwango
Umepakuliwa mara 6 | Umetazamwa mara 25
Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 22 Mwaka A
Kiitikio:
Ee Bwana, Ee Bwana (Bwana) Ee Bwana Mungu wangux2 NAfsi yangu inakuonea kiu (nafsi yangu) inakuonea kiu inakuonea kiu
Viimbilizi
1. Ee Mungu Mungu wangu nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu,
Mwili wangu wakuonea shauku, katika nchi kame isiyo na maji
2. Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, nizione nguvu zako na utukufu wako,
Maana fadhiliz ako ni njema kuliko uhai, midomo yangu midomo itakusifu
3. Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai, kwa jina lako nitaiinua mikono mikono yangu,
nafsi yangu itakinai kama kushiba nafuta na vinono, kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
4. Maana wewe umekuwa msaada wangu na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia
nafsi yangu nafsi yangu imekuandama sana, Mkono wako wa kuume unanitegemeza