Mtunzi: Wolford P. Pisa
> Mfahamu Zaidi Wolford P. Pisa
> Tazama Nyimbo nyingine za Wolford P. Pisa
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Wolford Peter Pisa
Umepakuliwa mara 5 | Umetazamwa mara 31
Download Nota Download MidiKIITIKIO:
Mfanyieni Bwana shangwe dunia yote, x2
mtumikieni Bwana kwa furaha, njoni mbele zake kwa kuimba x2
MASHAIRI
1. Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu wetu, ndiye aliyetuumba sisi tu watu wake,
na kondoo wa malisho na kondoo wa malisho yake.
2. Kwa kuwa Bwana ndiye mwema, na rehema zake ni za milele,
na uaminifu wake vizazi na vizazi.