Ingia / Jisajili

Wimbo Ulio Bora

Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga

Makundi Nyimbo: Ndoa

Umepakiwa na: David Wasonga

Umepakuliwa mara 12 | Umetazamwa mara 38

Download Nota
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

Inuka mpenzi wangu, wewe unipendezaye, njoo twende zetu waridi la moyo wangu, jipambe mavazi yako, jipambe kwa manukato, ujipambe kwa utu wema kwa upole na utulivu (x2)

Mashairi:

1. Kama yunguyungi katikati ya michongoma, ndivyo ulivyo mpenzi wangu, kama mbuzi washukavyo katika milima ya Gileadi, ndivyo ulivyo kati ya wasichana.

2. Kama mtofaa katika miti misituni, ndivyo ulivyo wewe kati ya wavulana wote.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa