Mtunzi: Beatus M. Idama
> Tazama Nyimbo nyingine za Beatus M. Idama
Makundi Nyimbo: Mama Maria
Umepakiwa na: Beatus Idama
Umepakuliwa mara 6 | Umetazamwa mara 43
Download Nota Download Midi
PAMOJA NA MALAIKA
1. Pamoja na malaika Maryamu Mama wetu,
Kuimba sifazo twataka zipende nyimbo zetu;
Maryamu ee zipokee hizo zako heshima, twakuimba twakuomba utuelekee Mama.
2. Mazuri ya ulimwengu si kitu mbele zako,
Hata nyota za uwingu zavia mbele zako;
Maryamu ee zipokee hizo zako heshima, twakuimba twakuomba utuelekee Mama.
3. Bikira usiye mfano sifazo kuzitaja,
Sitoshi haba maneno kubwa yako daraja;
Maryamu ee zipokee hizo zako heshima, twakuimba twakuomba utuelekee Mama.